Marekani yamtibua Balozi wa Ukraine nchini Afrika Kusini

NA DIRAMAKINI

BALOZI wa Ukraine nchini Afrika Kusini, Liubov Abravitova amesema ubalozi wake unaomba mkutano wa dharura na Waziri wa Ulinzi, Thandi Modise.
Balozi wa Ukraine nchini Afrika Kusini, Liubov Abravitova. (Picha na AFP/Phill Magakoe).

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na eNCA uamuzi huo umefikiwa kufuatia tuhuma zilizotolewa na Balozi wa Marekani,
Reuben Brigety kwamba Afrika Kusini iliipatia Urusi silaha.

Balozi Reuben Brigety alisema Alhamisi asubuhi kwamba, Marekani inaamini kwamba uhamishaji wa silaha ulifanyika wakati wa zoezi la majini ambalo Urusi iliendesha katika maji ya Afrika Kusini mnamo Februari.

Afrika Kusini imedumisha msimamo wa kutoegemea upande wowote juu ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, lakini tuhuma ya madai hayo inataka kudhoofisha msimamo huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news