MBUNGE PROF.MUHONGO APELEKA MAOMBI KWA HALMASHAURI YA MUSOMA IKAMILISHE MIRADI YA MAENDELEO

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Prof. Sospeter Muhongo, ameiomba Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ikamilishe miradi mikubwa ya maendeleo iliyopo ili iwanufaishe wananchi. 
Prof. Muhongo ameyasema hayo Mei, 12 2023 kupitia taarifa aliyoitoa. Ambapo amesema, kukamilika kwa miradi hiyo kutatatua changamoto za Wananchi katika maeneo yao. 

Moja ya miradi hiyo ni ujenzi wa hospitali ya wilaya inayojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero Kijiji cha Suguti ambapo serikali imetoa fedha nyingi za ujenzi huo.

Amesema, kukamilika kwa hospitali hiyo kutasaidia huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kupata huduma karibu na kuondokana na kutembea umbali mrefu.

Mradi mwingine mkubwa ni ujenzi wa makao makuu ya halmashauri inayojengwa hapo hapo Kwikonero ili iweze kukamilika.

Muhongo amesema vipo vituo vya afya vilivyojengwa chini ya kiwango virekebishwe na kukamilishwa ambavyo ni vile vya Mugango na Bugwema ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini. 

Amehimiza halmashauri itekeleze ipasavyo miradi ya maendeleo ya wanavijiji kwa kutumia mapato yake ya ndani ambayo juhudi za makusanyo zinapaswa kufanyika kuongeza makusanyo kwa ajili ya maendeleo.

Mbunge huyo ametoa rai kwa halmashauri hiyo ijiepushe kupata hati chafu ambazo hazikubaliki kwa wananchi na kupata maelezo ya hati hizo.

"Halmashauri itambue michango ya wadau wa maendeleo ikiwemo ya mbunge na michango ya wanavijiji (nguvukazi zao) kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa vijijini mwetu na kuomba ripoti za matumizi mabaya ya fedha za umma zitolewe haraka,"amesema Prof. Muhongo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news