NA MWANDISHI WETU
Morogoro
WAKAZI wa Mkoa wa Morogoro wameendelea kuneemeka na miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuunganishiwa umeme katika huduma za kijamii kama shule na zahanati huku umeme ukitumika pia kuinua uchumi wa maeneo husika kutokana na kuanzishwa kwa baadhi ya biashara zinazotegemea zaidi upatikanaji wa huduma hiyo.
Pichani ni Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bi. JANETH MBENE walipotembelea baadhi ya huduma za kijamii zilizofaidika na Miradi ya umeme vijijini kama shule na zahanati ili kujionea namna inavyowafaidisha wakazi wa Mkoa wa Morogoro, Mei 11, 2023.