Musoma Vijijini kuandika historia kupitia kilimo kikubwa cha umwagiliaji

NA FRESHA KINASA

BONDE la Bugwema na Bonde la Suguti yaliyopo katika Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara yako kwenye bajeti ya Wizara ya Kilimo ya mwaka 2023/2024 iliyopitishwa na Bunge siku ya Mei 9, 2023 ili kuwezesha kilimo cha umwagiliaji kufanyika jimboni humo.
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Prof. Sospeter Muhongo kupitia taarifa yake. Ambapo amesema, usanifu utafanyija na baadae miundombinu ya umwagiliaji itajengwa.

"Mabonde yetu hayo mawili (Bugwema na Suguti) yako kwenye bajeti hiyo. Usanifu utafanyika na baadae miundombinu ya umwagiliaji itajengwa," amesema Prof. Muhongo na kuongeza kuwa."Kilimo kikubwa cha umwagiliaji kinaingia jimboni kwetu,"amesema. Prof. Muhongo.

Akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo siku ya Mei 8, 2023 bungeni jijini Dodoma Prof. Muhongo aliishauri Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kujikita katika kilimo cha umwagiliaji ili kuwezesha upatikanaji wa mkubwa wa chakula nchini, upatikanaji wa ajira, pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Bwire Juma mkazi wa Nyegina katika Jimbo la Musoma Vijijini akizunguma na DIRAMAKINI kwa njia ya simu amesema, Bonde la Bugwema na Bonde la Suguti yana mchango mkubwa sana katika kuchochea maendeleo ya ukuaji wa uchumi kwa wananchi jimboni humo na mkoa wa Mara kwa ujumla.

Amepongeza hatua ya serikali kuyaweka katika bajeti ya mwaka 2023/2024 kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji huku akisema ni faraja na neema kubwa kwa wananchi.

"Nimshukuru Prof. Muhongo kwa kuendelea kutuwakikisha vyema sana wana Musoma Vijijini Bungeni, nilimsikiliza akitoa ushauri kwa Serikali bungeni juu ya kilimo cha umwagiliaji. Ninaamini kabisa kilimo hicho kikifanyika nchini uzalishaji utaongezeka na sekta ya kilimo itakuwa na mchango mkubwa katika maendeleo badala ya kutegemea mvua kwani mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa yakiathiri uzalishaji hasa mvua kutokuwa za uhakika,"amesema Bwire Juma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news