NA FRESHA KINASA
SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan inatarajia kujenga barabara ya Musoma-Makojo-Busekera mkoani Mara kwa awamu mbili.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 22, 2023 na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mheshimiwa Prof.Sospeter Muhongo ambapo utekelezaji huo unatarajiwa kuanza kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, barabara hiyo ina urefu wa kilomita 92 ambapo sehemu zenye lami Musoma Mjini-Buhare ni kilomita 5.9 ambapo eneo lote hilo liko ndani ya Manispaa ya Mji wa Musoma.
Aidha, Kusenyi-Kwikonero ni kilomita 5 na eneo lote hilo liko Musoma Vijijini huku kwa mujibu wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 barabara yao imepewa kilomita 40 katika awamu ya kwanza.
"Wananchi na viongozi wote wa chama na Serikali wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaishukuru sana Serikali yetu kufanya maamuzi mazuri ya kukamilisha ujenzi wa barabara hili (Musoma-Makojo-Busekera) kwa awamu mbili.
"Asante sana Rais wetu, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza kilio chetu cha miaka mingi na hatimaye kuamua kutatatua tatizo hili sugu. Tunashukuru sana,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.
Pia, kwa mujibu wa taarifa hiyo awamu ya kwanza kilomita 40 tayari ujenzi wa barabara hiyo ulishaanza kwa kujenga kilomita tano kuanzia Kijiji cha Kusenyi kuelekea Kijiji cha Makojo hadi kijijini Busekera (mwisho wa barabara).
"Ujenzi wa kilomita 40 uendelee kwa mpangillio huo huo, yaani, kuanzia Kitongoji cha Kwikonero (Kijiji cha Suguti) kuelekea Kijijini Busekera tusiache vipande vipande,"imesisitiza taarifa hiyo.
Wakati huo huo, katika awamu ya pili taarifa hiyo imefafanua kuwa, ujenzi utaanzia kijijini Kusenyi kuelekea Musoma Mjini. "Ushauri,achukuliwe Mkandarasi mzoefu, na anayejitosheleza kwenye vifaa vya ujenzi.Ujenzi uanze haraka baada ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2023/2024 kuanza kutumika, yaani Julai Mosi, 2023,"imeongeza taarifa hiyo.