Mwinjilisti Alphonse Temba aibua hoja nzito kuhusu Soko la Kariakoo

NA DIRAMAKINI

MUHUBIRI na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonse Temba ameishauri Serikali kuangalia namna bora ya kuandaa mpango mkakati wa kuja na ujenzi wa soko jipya la Kimataifa la Kariakoo ili liweze kukidhi mahitaji ya sasa na siku zijazo.
Temba ambaye pia ni mbobezi katika masuala ya uchumi na biashara amesema, Soko la Kimataifa la Kariakoo ni moja ya fursa kubwa nchini ambapo Serikali ilipaswa kujua ni moja ya ongezeko la uchumi kimapato na fursa kwa ajira kwa watanzania wengi. 

"Hivyo ikumbuke kuwa Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo ni sehemu ndogo sana ilikuwa imepangwa kisoko na eneo kubwa ilikuwa nyumba za Wahindi, Wamanyema na Waarabu, lakini baada fursa za kibiashara kuzidi ndipo umaarufu mkubwa wa Soko la Kariakoo ulivyoongezeka kila kukicha, miaka 20 iliyopita hali ya biashara siyo sawa na sasa. Watu wameongezeka, lakini maduka ni madogo sana na joto ndani ni kubwa sana leo.

"Pia mazingira ya kibiashara siyo mazuri, uchafu na msongamano wa watu unazidi kuwa mkubwa sana, pamoja na Serikali kufungua masoko kadhaa pembezoni mwa mji wa Dar es Salaam, lakini tofauti ni kuwa Soko la Kariakoo linabaki kuwa soko la tofauti kwa sababu kadhaa ikiwepo na wageni toka nchi kumi zinazotuzunguka kufika kama Dubai kununua vfaa vya bei poa. 

"Hivyo, Serikali lazima itambue kuwa miaka 50 ijayo lazima iandaliwe New Kariakoo ambayo itajengwa rasmi kama soko na kuwa na njia za hata mita 20 kwa tofauti ya maduka pia kuwa na bustani na miti ya vivuli ndani ya maeneo ya soko hilo.

"Nashauri Serikali kuangalia sasa kuandaa eneo lingine kubwa, kuandaa Soko kubwa la Kariakoo ambalo miaka 100 ijayo mataifa ya nje yatanufaika na litakuza uchumi wa nchi.
"Ninaishauri Serikali eneo la Vigwaza Mizani kwenda Mbala Chamakweza Chalinze karibu na Bandari Kavu ya Kwala katika eneo la Serikali la Narco,pajengwe soko la kisasa la Kariakoo ambalo zaidi ya ekari 200 zitengwe na maaeneo ya maegesho ya magari makubwa yatengwe. 

"Hali hiyo itaongeza ajira zaidi ya watu milioni moja na mataifa zaidi ya kumi yatanufaika pia, masoko yatakuwa na nafasi kubwa na stoho ndani ya kila duka ambapo hata mizigo ya fuso inaweza kuingia kwa mara moja na TRA wanakuwa na nafasi zuri ya ukaguzi kwa mizigo iliyoko sokoni.

"Soko la Kariakoo litaendelea, lakini litapunguziwa huitaji hasa wa Kimataifa na Serikali sasa imeamua kuufaanya mji wa Kwala kuwa wa kibiashara, hivyo itakuwa ni eneo sahihi sana. 

"Pia mazao yanayotoka mikoani hayana budi kwenda Dar es Salaam tena, hivyo kiwanda cha nyama kilichoshindikana cha Ruvu Darajani kigeuzwe soko la mazao kama vile ilivyo Kibaigwa ambapo vipikapu vitazoa mazao toka huko na kusambaza katika masoko ya Dar. 

"Hii itasaidia vijana zaidi laki tano kupata ajira na kuinua vipato vya familia, mambo haya pia yaanze mapema sana kunusuru hata magonjwa ya milipuko Dar, na matishio ya kigaidi kutokana na msongamano wa watu Dar, barabara za masoko ziwepo za mita mpaka 20 hili hata hajali za moto gari za Zimamoto na Uokoaji zipate nafasi ya kupita vizuri.

"Ziko hathari nyingi za kibinadamu kwa soko la Kariakoo kwa sababu haliko katika viwango vya kisoko hila imetokea kwa hali ya kibiashara. Naomba ushauri huu ufanyiwe kazi ili kunusuru maaafa na majanga huko mbeleni,"amefafanua Mwinjilisti Temba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news