Nabii Rolinga, Meseret Taye waendelea kuachilia upako wa uponyaji

NA MWANDISHI WETU

KANISA la Omega Ministries Church of All Nations (OCAN) ambalo lipo Mbezi Beach Africana jijini Dar es Salaam chini ya mtoto wa Mungu, Nabii Samson Samwel Rolinga limempokea Nabii Meseret Taye kutoka Ethiopia ambaye anaendelea na Kambi Maalum ya Uponyaji kanisani hapo.
Nabii Taye aliwasili nchini na kupokelewa na Nabii Roliga siku ya Mei 25, 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kliniki hiyo ya uponyaji inafanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia Mei 26, 2023 hadi Mei 28, 2023 katika viwanja vya Kanisa la Omega lililopo Mbenzi Beach Africana jijini Dar es Salaam.

Tangu kuanzishwa kwa kliniki ya uponyaji mwaka 2019 na huu ni msimu wa tatu, hivyo msimu huu wa Kliniki ya Uponyaji (Healing Clinic) mwaka 2023 utaongozwa vizuri na mtoto wa Mungu Nabii Rolinga akiwa na ndugu yake katika Kristo Nabii Meseret Taye kutoka Ethiopia.
Kliniki ya uponyaji ya msimu huu itakuwa na miujiza na matendo makuu ya mungu ambayo yanabadilisha historia ya maisha ya watanzania na kizazi chake chote hivyo mtanzania anatakiwa wawalete wagonjwa wa kila aina na wenye shida mbalimbali na watafunguliwa na Yesu kristo. 

Mtoto wa Mungu Nabii Rolinga amesema kuwa, siku tatu za kliniki ya uponyaji inatoa fursa kwa wagonjwa wa kila aina na wenye shida mbalimbali kupata suluhisho wa matatizo yao kutoka kwa waatalam wa afya na muujiza wa Yesu kristo. 
"Kliniki ya uponyaji ni kliniki itakayowajumuisha waatalam mbalimbali wa afya na watoto wa mungu katoa huduma ya kiroho itakayowaponya wagonjwa na watu wenye shida mbalimbali,"alisema Nabii Rolinga. 

Nabii Rolinga aliongezea na kusema kuwa yeye na Nabii Meseret Taye kwa pamoja ni zao la Nabii TB Joshua. 
Naye Nabii Meseret Taye kutoka Ethiopia amewashukuru OMEGA Ministries Church of All Nations kwa kuandaa kliniki hiyo muhimu kwa uponyaji kwa wagonjwa na wenye shida mbalimbali. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news