NA DIRAMAKINI
TIMU ya Nkansi FC imeibuka mshindi katika katika hitimisho la Mashindano ya Polisi Jamii Cup yaliyofanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.
Katika mashinano hayo yalishindanishwa kati ya timu nne ambazo ni Nkansia FC,Kalambo FC,Sumbawanga FC na Laela FC. Nkansi FC waliibuka mshindi kwa kuifunga Laela FC magoli mawili.
Mgeni rasmi katika mashindano hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Mheshimiwa Queen Cuthbert Sendiga ambapo aliwapongeza washindi na kuwapa zawadi ya shilingi 150,000, jezi jozi moja na cheti cha pongezi.
Naye ACP Mashenene wakati anahitimisha mashindano hayo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa aliwaasa vijana kutumia muda wa ziada kufanya mazoezi ili kujiepusha na vitendo vya uhalifu.
Wakati huo huo, Mkuu wa mkoa Rukwa aliahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa katika kuendeleza ushirikiano na raia ili kuiweka jamii karibu.