OUT yatembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Arusha

NA DKT.MOHAMED OMARY MAGUO

CHUO Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimepata fursa ya kutembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika Mkoa wa Arusha na kuzungumza na watumishi juu ya huduma na programu mbalimbali zinazotolewa na OUT.

Ziara yetu iliyoongozwa na Dkt. Nangware Msofe ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha OUT cha Mkoa wa Arusha akifuatana na Dkt. Mohamed Maguo na Mwalimu Rosemary Makiya tulipokelewa vizuri na Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Mkoa wa Arusha ndugu Philipo Msisi.

Hakika, yalikuwa ni mapokezi mazuri sana na tumezungumzia OUT kwa mapana yake kama ifuatavyo:

Mosi: Tumewaeleza watumishi wa TMA kwamba OUT ni Chuo Kikuu cha Umma kilichoanzishwa kwa sheria ya Bunge namba 17 ya mwaka 1992. 
 
OUT ina matawi katika mikoa yote ya Tanzania Bara na vituo vya uratibu Unguja, Pemba, Kahama na Tunduru. Hivyo watumishi wa TMA waliopo katika maeneo yote hayo wanaweza kujiendeleza kupitia OUT.

Pili: Tumewaeleza watumishi wa TMA kwamba OUT inatoa elimu bora kwa mifumo ya kisasa ya MOODLE Platform, Mihadhara mbashara kwa ZOOM, What's App Kimbwette, Telegram Kimbwette na ZOOM Kimbwette. 
 
Pia, tuna vitabu vya kujisomea vya nakala ngumu, mafunzo kwa vitendo na mafunzo ya ana kwa ana.

Tatu: Ada za masomo kupitia OUT ni gharama nafuu sana kwa watumishi kuweza kujiendeleza wakiwa kazini. 
 
Ada hulipwa kwa awamu awamu kulingana na Units ambazo mwanafunzi amesajili katika mwaka husika wa masomo.

Nne: Mwanafunzi anaweza kufanya mitihani katika vipindi 4 kwa mwaka na akachagua kipindi ambacho atakuwa ameshasoma na kujiandaa vizuri kufanya mitihani yake. Mwanafunzi halazimishwi kufanya mitihani ikiwa bado hajajiandaa kikamilifu.

Tano: Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa mkoa wa Arusha, ametupatia ushuhuda kwamba, yupo mtu mmoja ambaye ni wakili maarufu hapa jijini Arusha ambaye alisoma Shahada ya Sheria ya OUT na kisha akaenda Shule Kuu ya Sheria Tanzania na kumaliza mitihani yake na kufaulu katika kikao kimoja. 
 
Wakili huyo ni mbobezi tena nguli katika uga wa sheria hapa nchini. Hakika, tumefurahi sana kusikia hayo na tukamwambia mkuu kwamba wapo wengi sana wa aina hiyo na OUT tunajivunia sana.

Hitimisho

Tunapenda kutoa shukurani za dhati kwa uongozi wa TMA Arusha kwa kutupatia fursa ya kuwapatia maelezo kuhusu OUT ili waweze kutumia fursa zinazotolewa na chuo hiki. Maelezo katika andiko hili yatawafaa pia watu wote wanaopenda kujiendeleza huku wakiwa wanaendelea na kazi zao na biasahara zao bila kuziacha.

WENU

Dkt. Mohamed Omary Maguo
Mhadhiri Mwandamizi
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Arusha
18/05/2023

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news