PARIS-Papa Francis amemvua upadri mzaliwa wa Rwanda ambaye amekuwa akihudumu kama kasisi Kaskazini mwa Ufaransa kwa takribani miongo mitatu.
Taarifa inayosambazwa mtandaoni iliyotiwa saini na Askofu wa Évreux inasema kwamba Wenceslas Munyeshyaka (64), "anapoteza moja kwa moja haki za ukasisi" na "amezuiliwa" kutumikia "mahali popote" kama kasisi.
Ofisi ya Dayosisi ya Evreux imeithibitishia BBC uhalisia wa taarifa hiyo ambayo inasema kuwa inatokana na agizo la Papa la Machi.
Munyeshyaka ambaye alikimbilia Ufaransa baada ya mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994, hajazungumzia uamuzi huo.
Alisimamishwa kazi na Dayosisi ya Evreux mnamo Desemba 2021 baada ya kuibuka kuwa amekiri kisheria kuwa baba wa mvulana wa miaka 10.
Munyeshyaka alitawazwa kuwa kasisi nchini Rwanda mwaka 1992 ambapo anatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya mamia ya Watutsi waliokuwa wamekimbilia kanisani kwake katika mji mkuu wa Kigali wakati wa mauaji ya kimbari.Mahakama nchini Ufaransa zimemuondolea mashtaka ya mauaji ya halaiki.(BBC)