NA MWANDISHI WETU
CHUO Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kinatarajia kuanza ujenzi wa kituo cha kisasa katika eneo la ekari 105 lililopo Bungo Kibaha Mkoa wa Pwani kuanzia mwezi Julai 2023.

Prof. Ngaruko amesema kwamba, "OUT imejipanga kujenga kituo cha kisasa cha utafiti, uvumbuzi, ubunifu na ukarimu Bungo Kibaha kuanzia Julai 2023.
"Hii ni kutokana na mradi wa Mageuzi ya Uchumi kupitia Elimu ya Juu (HEET) unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lengo la kituo hicho ni kwa ajili ya kutoa wahitimu na watafiti ambao watakuwa na uwezo mkubwa wa kubuni, kuibua na kuanzisha ajira nyingi kwa jamii ya Watanzania na kisha kuchochea katika kukuza uchumi wa nchi yetu. Tayari kazi ya maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho inaendelea vizuri."

Vilevile, Prof. Ngaruko ameongeza kwamba, wafanyakazi katika uwekezaji huo mkubwa watakuwa ni wanafunzi wa OUT wanaosoma programu za Astashahada, Stashahada, Shahada, Shahada za Umahiri na Uzamivu.
Sehemu kubwa ya vitu vitakavyotumika ndani ya kituo hicho ikiwemo chakula na mahitaji mengine yote yanatarajiwa kuzalishwa hapo hapo.
