Prof.Muhongo adhamiria kupaisha elimu Musoma Vijijini

NA FRESHA KINASA

JUHUDI za kuimarisha sekta ya elimu katika Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara zinaendelea kufanywa na Mbunge wa jimbo hilo, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo.
Ambapo, anatarajia kuendesha harambee kwa ajili ya ujenzi wa sekondari nne mpya jimboni humo na kufanya mikutano na wananchi ili kuweka mikakakati madhubuti ya pamoja juu ya umuhimu wa sekta hiyo katika kuchangia kuleta maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa leo Mei 25, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa jimbo hilo ambapo shule hizo zitafunguliwa mwakani Januari 2024.

"Vijiji vinavyojenga sekondari mpya zitakazofunguliwa Januari 2024 ni Nyasaungu Kata ya Ifulifu, Sekondari ya pili, Muhoji Kata ya Bugwema, Sekondari ya pili Wanyere Kata ya Suguti, Sekondari ya pili, Kisiwa cha Rukuba

Kata ya Etaro, Sekondari ya pili. Mbunge wa Jimbo, Prof. Sospeter Muhongo, atatembelea vijiji vilivyo kwenye ujenzi wa sekondari zao."imeeleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza kuwa.

"Mbunge Mheshimiwa Prof. Muhongo ataongea na wananchi wa maeneo hayo na baadae atapiga harambee za kuchangia ujenzi wa sekondari hizo. Viongozi wa Vijiji na Kata watakaribisha Wadau wa Maendeleo kuchangia ujenzi wa sekondari zao," imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo imebainisha kuwa, jimbo hilo la Musoma Vijijini lina jumla ya kata 21, zenye jumla ya Vijiji 68 na vitongoji 374. Huku jumla ya shule za Sekondari za kata zikiwa ni 25, na binafsi shule 2.

Shabani Paul na Walecce Sadick wakazi wa Kata ya Mugango katika Jimbo la Musoma Vijijini wakizungumza na DIRAMAKINI kwa nyakati tofauti wamepongeza juhudi za Mbunge wao Prof. Muhongo katika kuhakikisha elimu inaleta mafanikio ikiwemo juhudi zake za kuchangia ujenzi wa shule za Sekondari, ujenzi wa maabara, kusaidia kulipa walimu wa masomo ya Sayansi, na msisitizo wake kwa wazazi/walezi kusomesha watoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news