Prof.Muhongo apendekeza jambo muhimu Sekta ya Elimu

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Prof.Sospeter Muhongo ametoa ushauri kwenye uboreshaji wa elimu nchini.

Katika ushauri wake,Prof. Muhongo ameeleza umuhimu wa kuwepo maktaba na maabara kwenye shule zetu vilevile ameeleza umuhimu wa Space Sciences and Technologies (Sayansi ya Anga na Teknolojia).

Prof. Muhongo ametoa ushauri huo bungeni jijini Dodoma Mei 17, 2023 wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2023/24.

"Waheshimiwa wabunge,mimi natoa ushauri wangu nilikuwa sipo nimesikiliza na ukweli ni kwamba elimu yetu iko kwenye hali mbaya lazima kwanza tukiri hivyo. Lakini hakuna wa kumlaumu ni sisi wote tukitaka kulaumu mtu ni kama hatujui tunalolifanya.

"Kwanza kabisa Mheshimiwa Spika pendekezo langu, ni kwamba elimu ya awali kuipeleka TAMISEMI imekaa TAMISEMI kwa muda matokeo yake sio mazuri. Maana yake huko nyuma tulikopeleka madaraka ya ndani si ndiko tulifanya mabadiliko sasa tukifanya tathmini hayajazaa matunda.

"Mimi napendekeza sababu turudi nyuma, Wizara ya Elimu inarudisha tena mambo ya elimu yawe ndani ya wizara moja. Inakuwa ngumu sana eti shule ya msingi (primary) inakuwa na Waziri wake, Ofisi zake ikifika (University) chuo kikuu nayo ya kwake baadae mnalaumiana napendekeza Profesa lipelekwe kwenye cabinet, aifikirie muwe na wizara inaitwa Wizara ya Elimu Sayansi Utafiti na Ubunifu.

"Yaani iwe Ministry of Education Science Research and Innovation' huna haja ya kutaja teknolojia sababu teknolojia inakuwa ndani ya innovation."

"La pili, kwenye shule zetu Profesa na TAMISEMI lazima mkae chini mkubaliane kwamba ili tuwe na elimu nzuri na inaweka msingi mzuri lazima kila shule vyumba vya madarasa viwe na wanafunzi wangapi."

"Kwa hiyo home work ya kwanza turudi nyuma tuone tunarekebisha, huko nyuma enzi yangu shule ya msingi tulikuwa wanafunzi 45, sekondari wanafunzi 35, high school 25, sasa hebu turudi huko kwanza. Hii mitaala hata ukiwa nayo mizuri kiasi gani wanafunzi wakarundikana madarasani hutafaulu."

UMUHIMU WA MAABARA

"Halafu shule yoyote ile inayoitwa shule duniani kote na mimi nimezunguka kweli kweli duniani sijawahi kwenda shule nikakuta haina maabara, haina maktaba hiyo ni shule gani?.

"Mimi sasa hivi Musoma Vijijini nimeweza kujenga maktaba kwenye shule tatu za msingi watu wananishangaa, wanasema Prof. Mbona unang'ang'ana kujenga maktaba katika shule za msingi".

"Ninaomba wanaoshughulika na elimu wahakikishe kila shule ina maktaba kule tunakokwenda wataweka kompyuta zenye uwezo mkubwa na spidi.

"Hata hivi vitabu mnavyonunua sasa hivi vinatolewa bure sasa kama huna kompyuta hizi maktaba lazima ziwe na kompyuta kusaidia wanaoweza kupata vitabu vya bure ambavyo sasa hivi vinagawiwa bure huko duniani. Lazima shule iwe na maabara hilo ni tatizo kubwa naomba hilo lirekeboshwe."

ELIMU YA JUU

"Hii Profesa inakuhusu wewe, hii COSTECH (Tume ya Sanyasni na Teknolojia Tanzania) tuliyonayo hata tukimwaga humo fedha nyingi muundo wake imekaa kama Idara ya Wizara, COSTECH haipaswi kuwa hivyo, kwanza jina lenyewe lazima libadilishwe iitwe 'National Research Innovation Foundation iweke mkazo kwenye utafiti na ubunifu na yenywe ianze kufanya rating ya wasomi."

"Haiwezekani maprofesa wote hawalingani, na madaktari wote hawalingani. Sasa hatuna rating hatuna profesa Grade A, au B, pia hatuna daktari grade A, au D, kila mtu anaibuka tu na Tittle daktari inabidi wengine wale ambao ni wa halali wakae kimya.

"Hii kazi lazima tuiachie 'Nation Research Innovation Foundation' na duniani kote, foundation zimefanya vizuri uende Marekani au Africa Kusini na wanapata fedha wanakuwa na watu wengi."

VYUO VIKUU

"Hapa Profesa lazima uache Legacy kwamba hii Wizara ilikaliwa na Profesa, lazima uingie kila chuo tatizo letu sasa hivi ni moja ndio maana ukichukua vyuo vya Tanzania hakuna ambacho kiko 10 bora kwa Afrika, hatumo.

"Inamaanisha kwamba, utafiti kwenye vyuo vyetu umerudi chini mimi bado napokea machapisho kila nikicheki Tanzania naona hamna. Tuko chini, Profesa kaa na Ma-chancellors wako watu wameanzisha majarida sababu ya promotion na yatazidi kudidimiza kweli kweli elimu ya Tanzania.

"Siku moja Mwalimu alitutembela, Nilisoma Dar es Salaam, Chancellor alikuwa Nyerere akaja pale chuoni alizoea kuonana na wafanyakazi nami nilikuwa naanza kazi. Akasimama mtu mmoja senior akasema hiki chuo kina upendeleo sana mimi sijapandishwa cheo.

"Mimi sikujua kwamba Mwalimu alimpa scholarship kwenda kusoma Marekani kaongea Mwalimu akajibu akatuambia wote kwamba mimi nilikuwa nadhani mtu kuwa Profesa mnamhakikisha kweli kweli na anastahili kweli kama ni suala la mishahara wapandishieni tu mishahara, lakini msiwape hizi Titles.

"Sasa vyuo vyetu vimefikia hatua hata idara zinakuwa na majarida hizo ni for promotion. Niombe utakapokaa na Ma- vice Chancellors wako Mheshimiwa Profesa waambie kila Chancellor aje na chapisho lake moja baada ya jingine mkikaa ambazo hazifai ni nyingi tu, mimi nimeshazifanyia utafiti.

"Waheshimiwa wabunge kitu kinaitwa CA au kingine kinaitwa IP impact factor hii CI maana yake ni kwamba je, hilo jarida unalolitumia wangapi wanafanya rejea zao. Wanaofanya utafiti Profesa Mkenda ukikuta zina impact fact ya 0.05 au (CI) nitakuomba Mheshimiwa Waziri tuje tuongee.

"Jarida mnazozitumia duniani hazijulikani kwa hiyo ni zetu hapa hapa lazima uzipige vita. Na mwisho kuna maneno matatu tuwekee mkazo ukiwa kwenye hiyo wizara Profesa ni 'Space Science and Technology na hiyo inaingia setelaiti lazima uanzishe research kubwa na elimu kubwa kwenye eneo la mbegu seed science si tunataka kwenda kwenye kilimo.

"Na mwisho ni Science and Nanotechnology hata wale wagonjwa wa TB duniani wameacha kutumia vidonge vingi. Siku hizi wanachukua kidonge saizi ya unywele inatibu TB huko ndiko dunia inakokwenda,"amesema Prof. Muhongo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news