NA DIRAMAKINI
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo amewatakia heri wafanyakazi wote nchini.
Aidha, Prof. Muhongo amewahimiza wafanyakazi na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu kwa ajili ya kujiletea maendeleo.
"Nawatakia wafanyakazi wote maadhimisho mema ya siku ya wafanyakazi duniani, tuendelee kufanya kazi kwa bidii kwa manufaa ya taifa letu," amesema Prof. Muhongo.