Programu ya AFDP kuchochea maendeleo Sekta ya Kilimo na Uvuvi

NA MWANDISHI WETU

KATIBU MKUU Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema Serikali imedhamiria kuendelea kuwekeza katika sekta ya kilimo na uvuvi kwa lengo la kuchagiza maendeleo kupitia miradi inayotekelezwa na program ya kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi ya AFDP nchini. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiangalia mimea mbalimbali kwenye maabara ya mimea wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa program ya kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na ofisi yake katika maabara ya mimea mbalimbali pamoja na kalakana ya wakala wa mbegu za kilimo (ASA) mkoani Morogoro.

Ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Morogoro Mjini na wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro alipotembelea na kukagua shughuli za utekelezaji wa program hiyo inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiangalia moja na mapipa ya kuhifadhia maji katika maabara ya kutotoresha vifaranga vya samaki katika Kituo cha Viumbe Maji (DAQ) kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa program ya kilimo na uvuvi ya AFDP inayoratibiwa na ofisi yake. 

Katika ziara yake ametembelea Taasisi za Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA),Taasisi ya utafiti wa Mbegu (TARI), Taasisi ya udhibiti Ubora wa Mbegu (Tosci) pamoja na kukagua kituo Cha Viumbe Maji(DAQ) Kingolwira ikiwa ni sehemu ya maeneo yanayotekelezwa na program hiyo.
Mtendaji Mkuu Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) Dkt. Sophia Kashenge akimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi mimea ya michikichi katika shamba la mbegu Msimba Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa program wa kuendeleza kilimo na uvuvi ya AFDP inayoratibiwa na ofisi yake.

Dkt. Yonazi amesema uwekezaji huu utachangia kuongeza uzalishaji katika kilimo na uvuvi hii inatoa fursa kuchangia uchumi wan chi yetu na kuifanya nchi kuwa na chakula cha kutosha.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiangalia moja ya mmea wa mchikichi katika shamba la mbegu Msimba Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, kushoto ni Mtendaji Mkuu Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) Dkt. Sophia Kashenge wakati wa ziara kukagua utekelezaji wa program wa kuendeleza kilimo na uvuvi ya AFDP.

Aidha, uwekezaji huu unasaidia wananchi kuendelea kujifunza katika maeneo yanayotekeleza miradi hii kujiletea maendeleo yao.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiangalia bango la taarifa za shamba la mbegu Msimba linalomilikiwa na Taasisi ya Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro alipotembelea kukagua utekelezaji wa program wa kuendeleza kilimo na uvuvi ya AFDP inayoratibiwa na ofisi yake.Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa ASA Dkt. Sophia Kashenge.

“Maeneo yanayotekelezwa miradi ya AFDP yataleta chachu kwa wananchi kujifunza na kujipatia maarifa yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi,”alisema Dkt. Yonazi.
Mtendaji Mkuu wa ASA Dkt. Sophia Kashenge akimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi eneo la shamba la mbegu Msimba linalomilikiwa na Taasisi hiyo pamoja na kisima cha maji katika eneo hilo (hakipo pichani) katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Naye Mtendaji Mkuu Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) Dkt. Sophia Kashenge alieleza kuwa, Serikali kupiia Ofisi ya Waziri Mkuu imeendelea kuwa na tija katika kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi kupitia miradi mbalimbali hivyo wataendela kuunga mkono jitihada hizo kwa vitendo huku alibainisha mafanikio yaliyofikiwa na taasisi yake.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akioneshwa ramani na Msimamizi wa shamba la Mbegu Msimba Bw. Samson Mollel alipotembelea ofisi za Wakala wa Mbeguza Kilimo (ASA) Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro wakati wa ziara hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na watendaji wa Ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Mbegu (TIRA) Ilonga alipowatembelea kujionea utekelezaji wa program ya kuendeleza kilimo na uvuvi ya AFDP katika Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news