Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na viongozi na wananchi wa Chwaka katika kuitikia dua ya kumuombea marehemu Simai Msaraka Pinja, ikisomwa na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume (kushoto kwa Rais) na kulia kwa Rais) ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na viongozi na wananchi wa Chwaka katika kuitikia dua ya kumuombea marehemu Simai Msaraka Pinja ikisomwa na Sheikh Abdalla Khamis Juma (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika kijijini kwao Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja lna kulia kwa Rais ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja, Mhe. Rashid Sima Msaraka, mtoto wa marehemu na kushoto kwa Rais ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Simai Msaraka Pinja, wakati wa maziko yake yaliyofanyika Mei 13, 2023 kijijini kwao Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia wananchi wa Chwaka na kutoa mkono wa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu Simai Msaraka Pinja, baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja siku ya Mei 13, 2023.(Picha na Ikulu).