Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi tarehe 23 Mei 2023 amehudhuria ufunguzi wa Jukwaa la Uchumi jijini Doha nchini Qatar ambapo viongozi mbalimbali duniani wamehudhuria ufunguzi huo akiwemo Rais wa Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame.
Kabla ya ufunguzi wa jukwaa hilo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alizungumza na Mhe.Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Amir wa Taifa la Qatar.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Qatar hutumia jukwaa hilo la biashara kila mwaka kujitangaza kiuchumi na kukaribisha wawekezaji mbalimbali.