NA MWANDISHI WETU
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amehudhuria dhifa ya chakula cha mchana iliyokuwa imeandaliwa na mfanyabiashara maarufu kutoka Qatar, Sheikh Faisal bin Qassim bin Faisal Al-Thani.
Mfanyabiashara huyo ni mmiliki wa hoteli 30 kubwa duniani na makumbusho ya Sheikh Faisal Bin Qassim Al Thani Museum ambayo yana vitu vingi vya kusisimua vya zamani.
Moja kati ya vitu vilivyomvutia Rais Dkt.Mwinyi ni noti ya zamani ya Zanzibar iliyotumika mwanzoni mwa mwaka 1916.
Mbali na noti hiyo, makumbusho hayo pia yanahifadhi aina mbalimbali za magari ya zamani, yakiwemo yale yaliyotengenezwa mnamo mwaka 1890.