NA GODFREY NNKO
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Mei 31, 2023 saa 7:30 mchana Ikulu jijini Zanzibar anatarajiwa kuzindua vikao vya pamoja vya Kamati ya Maridhiano kati ya Chama cha ACT Wazalendo na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa Mei 30, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Charles Hilary.

Amebainisha kuwa, "Vyama hivi vimeunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, ikiwa ni hatua muhimu katika kuendeleza mazungumzo na ushirikiano kwa manufaa ya wananchi.
"Uamuzi huu unadhihirisha dhamira ya CCM na ACT Wazalendo kufanya kazi pamoja ili kujenga Zanzibar na wananchi wake,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika uzinduzi huo, Mheshimiwa Rais Dkt,Mwinyi atatoa hadidu rejea ambayo itaelezea mpango wa vyama hivyo viwili na hatua zijazo za Serikali.