Rais Dkt.Ruto akaribisha wawekezaji, kutoa ardhi bure ujenzi nyumba nafuu

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Awamu ya Tano imejitolea kuifanya Jamhuri ya Kenya kuwa kivutio kwa kuwavutia uwekezaji ndani na nje ya nchi. Mheshimiwa Rais Dkt.William Ruto amesema,tayari Serikali imeweka na inaendelea kuweka motisha ili kuvutia wafanyabiashara wengi zaidi wa kigeni.

Pia amesema,Serikali inaboresha kituo chake cha pamoja ili kuwarahisishia wawekezaji kufanya biashara nchini. "Tumechukua hatua za kutekeleza mageuzi ili kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni," alisema.

Rais Ruto ameyabainisha hayo Jumatatu wakati wa kongamano la kibiashara lililowaleta pamoja wawekezaji kutoka Uholanzi lililofanyika The Hague nchini Uholanzi.

Aliwaambia wawekezaji hao kuwa, Serikali imesuluhisha marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kuondoa ukiritimba.

Rais pia alitoa wito kwa wawekezaji wa kigeni kuingiza fedha zao katika mradi wa nyumba za bei nafuu, huduma ya afya,biashara ndogo na za kati (MSMEs) na uchumi wa ubunifu.

Alibainisha kuwa nchi inakabiliwa na uhaba wa nyumba, hasa katika miji mikubwa."Tutatoa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo bure ili kupunguza gharama za uzalishaji," alisema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news