NA MWANDISHI WETU
RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Ban Ki-moon jijini Seoul, Korea Kusini.
Mheshimiwa Dkt. Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education) - GPE) yuko Seoul, Korea Kusini kwa ajili ya kukutana na viongozi wa Serikali na Mashirika Mbalimbali ya Korea Kusini kwa ajili ya kujadili mikakati ya kuendelea kuboresha elimu katika nchi zinazoendelea.

Rais mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Ban Ki-moon jijini Seoul, Korea Kusini siku ya Mei 11, 2023.