Rais Ramaphosa:Sisi sio nchi pekee duniani ambayo inatatizika na umeme

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Afrika Kusini,Cyril Ramaphosa amewataka wananchi kuvuta subira wakati Serikali ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu kuhusu changamoto ya nishati ya umeme, kwani changamoto hiyo inayakabili mataifa mengi kwa sasa.

Mheshimiwa Ramaphosa ameyabainsha hayo wakati akizungumza katika ziara yake ya KwaZulu-Natal, huku chama tawala kikijaribu kurejesha matumaini yaliyopotea kwa wananchi kabla ya uchaguzi wa 2024.

Amesema, Waziri wa Umeme anafanya kazi kwa bidii kutatua tatizo hilo."Sisi sio nchi pekee duniani ambayo inatatizika na umeme, nchi nyingine nyingi duniani zimepata changamoto moja au baadhi ya kuzalisha nishati," alisema.

Hivi karibuni, Rais Ramaphosa alimteua, Mheshimiwa Kgosientsho Ramokgopa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia umeme.

Waziri huyo amekuwa na jukumu la kusuluhisha mzozo wa sasa wa umeme unaokabili nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi wa kiviwanda barani Afrika.

Afrika Kusini inakabiliwa na tatizo kubwa zaidi la umeme kuwahi kutokea katika miongo kadhaa, huku umeme ukiwa unakatika mara kwa mara hadi saa kadhaa kwa siku.

"Kazi ya msingi ya waziri mpya itakuwa kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa umeme kama jambo la dharura," Rais Ramaphosa alibainisha hayo hivi karibuni baada ya kumteua waziri huyo.

Pia alisema,Waziri wa Umeme ataratibu idara na taasisi zote zinazohusika katika kukabiliana na mgogoro huo, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi na uongozi wa Shirika la Umeme la Afrika Kusini (Eskom) kwa ajili ya kuongeza kasi ya uzalishaji umeme kwa njia mpya nchini humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news