NA DIRAMAKINI
SERIKALI ya Jamhuri ya Kenya imejitolea kuwasilisha maeneo 25,000 ya kutolea bure huduma ya Wi-Fi kote nchini. Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt.William Ruto amesema hii itasaidia biashara ndogo ndogo, na za kati kujihusisha na biashara ya mtandaoni.
Pia amesema,huduma hiyo isiyo na waya pia itawapa vijana wa Kenya fursa ya kutafuta nafasi za kazi mtandaoni. "Kuna mamilioni ya fursa za mtandaoni ambazo vijana wetu wanaweza kutumia."
Mheshimiwa Rais Dkt.Ruto ameyasema hayo Ijumaa ya wiki hii wakati wa Maonesho ya Siku ya Madaraka (Madaraka Day) ambayo yalihusisha makundi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara ndogo ndogo, za kati, vyama vya ushirika na nyinginezo katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Embu.

Rais Dkt.Ruto pia alizindua Wi-Fi ya Bure ya Chuo Kikuu cha Embu. Waliohudhuria ni Naibu Rais Rigathi Gachagua, mawaziri Simon Chelugui, Moses Kuria, Eliud Owalo, Zacharia Njeru na Gavana wa Embu Cecily Mbarire miongoni mwa viongozi wengine.