Rais Ruto:Siwezi kuvumilia ufisadi, dhuluma kila Mkenya apate haki

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt.William Ruto ameiagiza Wizara ya Ardhi kuchukua jukumu la kuthamini ardhi kutoka kwa Tume ya Kitaifa ya Ardhi (NLC).

Amesema hatua hiyo inalenga kukomesha enzi zisizo za haki na ufisadi za tume katika ulipaji fidia ya ardhi. Pia amesema,sio sawa kwa NLC kuthamini ardhi na kufidia kwa wakati mmoja.

"Tunataka kuhakikisha kuwa kila Mkenya anafidiwa kwa haki," alisema. Rais Dkt.Ruto aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa ibada ya maombi katika Shule ya Upili ya Wavulana ya Isiolo akiwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua, Waziri wa Ulinzi Aden Duale, Magavana Mohamud Ali (Marsabit) na Abdi Guyo (Isiolo) na wabunge mbalimbali.

Rais amewataka viongozi kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kufanya kazi pamoja ili kukabiliana na changamoto zinazowakumba Wakenya.

"Hatuna muda wa kugombana na kubaguana, ni wakati wa kuwatumikia wananchi," alisema. Rais alisema serikali inaweka mipango na sera za makusudi za kutengeneza ajira kwa vijana na kuwaepusha na dawa za kulevya na maovu mengine.

"Hatuwezi kuwa taifa la walevi, lazima tuwe taifa la wanalofanya kazi," alisema. Naye Naibu Rais, Gachugua alisema serikali itawajibisha machifu na wakuu wa polisi kwa matumizi mabaya ya dawa za kulevya katika maeneo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news