REA yaendelea kuvifanya vijiji kuwa kama mijini

NA DIRAMAKINI

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuvifanya vijiji mbalimbali kikiwemo Kijiji cha Buhumbi kilichopo Kata ya Buhumbi wilayani Magu Mkoa wa Mwanza kuwa kama mijini kutokana na kasi yake ya kuviunganisha vijiji na huduma za umeme nchini.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Buhumbi, Mikael Dambalu Sahani ameonesha kuguswa na huduma za REA huku akisema, ujio wa umeme wa REA kijijini hapo unakwenda kuongeza hamasa na kuharakisha maendeleo.

"Napenda nishukuru kwa kutuletea umeme katika Kijiji changu cha Buhumbi,Kata ya Buhumbi. Nashukuru sana kwa kutuletea umeme, na hii miradi ya umeme wananchi wangu walikuwa na hamasa sana ya kupata umeme na kweli Serikali imeona inafaa ituletee umeme katika Kijiji cha Buhumbi, na hapo mimi mwenyekiti ninashukuru sana kwa kutuletea umeme katika Kijiji cha Buhumbi. Mimi kama Mwenyekiti nitashiriki na wananchi wangu ili kuhakikisha kila mji au kitongoji kinapata umeme na kila familia.

"Wataalamu wa umeme ninawaomba sana tushirikiane ili suala la kupata huu mradi wa umeme katika familia zetu. Kijiji changu cha Buhumbi kwanza kilikuwa chini sana zamani, sasa hivi Serikali imeona angalau kijiji changu kipate umeme, kwa kweli hata mimi ninashukuru sana, huu mradi ninaupokea kwa hali na mali."

Mwenyekiti huyo amefafanua kuwa, ujio wa nishati ya umeme kijijini hapo utarahisisha kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo mashine, kituo cha afya na nyinginezo ili kuharakisha maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news