Salim Njaidi:Nilitelekezwa kwa muuza genge nikiwa na miezi 11

NA DIRAMAKINI

MKAZI wa Pugu katika Halmashauri ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam,Salim Njaidi amesema akiwa na umri wa miezi 11 mwaka 1998 mama yake mzazi ambaye hamjui kwa sura wala jina alimtelekeza kwa mama muuza genge la matunda huko mkoani Mwanza.

Ni baada ya mama yake kununua tikiti na maembe katika genge hilo na kwenda chooni na kumuacha kwa muuzaji huyo.
Ameyasema hayo katika mahojiano kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, huku akidai kuwa,huenda mama yake alimtelekeza gengeni kutokana na ugumu wa maisha, lakini yeye binafsi anamtafuta na amemsamehe na anatamani kumuona ili amuite mama.

Pia, Salim ameeleza alipofika kidato cha pili ndio alijua kuwa wanaomlea sio ndugu zake wa damu baada ya mama muuza genge hilo kumweleza historia halisi ya maisha yake.

Amesema, hata hivyo mama muuza genge aliyemlea naye alikuja kufariki kwa ugonjwa wa shinikizo la juu la damu.

Vivyo hivyo, Salim amesema kuwa, jina la Salim alipewa na mama muuza genge, hivyo hajui jina lake la awali wala hamjui mama, baba, dada, mama mdogo, wala shangazi kwa maana ya ndugu zake wote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news