Serikali kuzingatia mafungu maalum ya fedha kwa WAVIU

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama amesema utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 pamoja na vipaombele vingine inazingatia pia mafungu ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) katika kila iwzara na taasisi.
Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Sera na Programu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Crispin Musiba akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.

Ameyasema hayo mapema leo 25 Mei 2023, katika Ukumbi wa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA).

Mhe. Mhagama, aliendelea kusema kuwa hii ni namna ambavyo Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kwa dhati kusaidia utekelezaji wa Afua za masuala ya UKIMWI nchini, kwa kuzingatia maeneo muhimu ikiwemo masuala ya lishe bora, dawa za kupunguza makali ya virusi na kuhakikisha mambo mengine yanayochangia ustawi wao kupatikana.
Akizungumzia suala la Sera ya Taifa ya UKIMWI ya mwaka 2001 Mhe. Mhagama alisema kuwa kuna kila Sababu ya Sera hiyo kufanyiwa mapitio na maboresho kwani ni ya muda mrefu na kuona, namna gani sekta zote zinaweza kushiriki katika suala hili ili kuweza kuyafikia malengo ya dunia ya kupunguza vifo, maambukizi na unyanyapaa ifikikapo 2030. 

"Niwahakikishie kwamba sisi kama Serikali tunaweza kusimamia kufikia malengo haya ya dunia.”amesisitiza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa NACOPHA Mwalimu Leticia Mourice alimpongeza Mhe. Waziri Jenista kwa uteuzi wake na pia kumshukuru kwa juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI, aidha aligusia kuhusiana na maandalizi ya Mdahalo wa Kitaifa kuhusu uhimilivu wa mwitikio wa jamii katika mwitikio wa Taifa wa UKIMWI ifikapo mwaka 2030.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Nchini na mjumbe wa Bodi ya NACOPHA Bi. Pudensiana Mbwiliza akitoa maelezo namna ya vijana hao wanavyonufaika na NACOPHA wakati wa kikao chao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) Mwalimu Leticia Mourice baada ya kumaliza Mazungumzo hayo.

Sambamba na hilo alizungumzia kuhusu, uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa, ambao unalenga utekelezaji wa NMSF5 (Mpango Mkakati wa Tano wa Kitaifa wa Kudhibiti UKIMWI) na alisisitizia umuhimu wa ushirikiano, katika kujenga mwitikio wa kijamii katika mapambano dhidi ya UKIMWI, akitolea mfano maeneo kadhaa muhimu ikiwemo Uhimilivu wa Kisera. 
Afisa Mtendaji Mkuu kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA), Bw. Deogratias Rutatwa akitoa maelezo kuhusu NACOPHA kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).

Awali, akizungumza katika mkutano huo Afisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA, Bw. Deogratius Rutatwa, aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuipongeza Serikali ya watu wa Marekeni (PEPFAR/USAID) kwa mchango wake mkubwa katika kufanikisha shughuli za mwitikio wa UKIMWI za NACOPHA na wadau wote wanaotekeleza suala la UKIMWI na kusema kuwa kuna haja ya kuwepo kwa mkakati endelevu na uhimilivu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news