Simba yaishusha daraja Ruvu Shooting FC kwa mabao 3-0

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Simba ya jijini Dar es Salaam licha ya kuonekana kutofanya vizuri katika baadhi ya michuano siku za karibuni imeandika rekodi ya kuwashusha daraja wajeda wa Ruvu Shooting kupitia kichapo cha mabao 3-0.

Winga wa Kimataifa, Pape Ousmane Sakho akitokea benchi kipindi cha pili aliifungia Simba SC mabao mawili katika mtanangeb huo.

Ni mtanage wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa usiku huu katika dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamanzi ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama aliifungia Simba SC bao la kwanza dakika ya 30, kabla ya Sakho kuongeza mawili dakika ya 72 na 90 ya mtanange huo.

Aidha, Jonas Mkude wa Simba SC katika mtanange huo alioneshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu mpinzani wake, William Patrick.

Dakika kadhaa kabla ya mchezo huo kocha mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera (Robertinho) alisema, wanahitaji ushindi katika nchezo huo ili kurudisha imani ya mashabiki.

“Tunahitaji ushundi kwenye mchezo huu tunajua kwamba hautakuwa mchezo rahisi lakini kwa uwezo wa Mungu tutafanya vizuri na nilisha zungumza na wachezaji wangu juu ya umuhimu wa mchezo huu,”alisema Robertinho.

Kwa matokeo hayo yanamaanisha Ruvu Shooting imeipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kuelekea mechi mbili za mwisho, kwani alama walizonazo haziwezi kuongeza chochote.

Aidha, Simba SC inafikisha alama 67 katika mchezo wa 28, nyuma ya Mabingwa watetezi, Yanga wenye alama 71 za mechi 27 ambao wanaweza kutawazwa kuwa mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo kama watashinda dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo ujao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news