NA MWANDISHI WETU
SERIKALI kupitia Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) inaendelea na ujenzi wa ofisi mpya pamoja na maabara katika Kata ya Mkolani Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.
Mkuu wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa, Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania, Bw. MIGUTA NGULIMI amesema, dhamira ya serikali ni kusogeza huduma karibu na wananchi na kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia huduma za vibali vya mionzi pamoja na ukaguzi wa watumiaji wa vyanzo vya mionzi.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania, Bw. PETER NGAMILO amesema serikali inaendelea na ujenzi wa maabara pamoja na ofisi Dar es Salaam na Zanzibar ili kurahisisha huduma kwa wananchi na kuhakikisha wapo salama katika matumizi ya mionzi na teknolojia ya nyuklia.