NA GODFREY NNKO
ZAIDI ya mataifa 30 duniani yanatarajiwa kushiriki katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayotarajiwa kuanza Juni 28, 2023 hadi Julai 13, 2023 ndani ya viwanja vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (SabaSaba) vilivyopo Barabara ya Kilwa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa mataifa ambayo tayari yamethibitisha kushiriki ni China, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE),Uturuki, Kenya, Ghana,India, Singapore, Syria, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,Indonesia, Rwanda, Algeria na Pakistan.

Hayo yamebainishwa leo Mei 19, 2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Biashara kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Fortunatus Mhambe wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya mamlaka hiyo zilizopo ndani ya viwanja hivyo.
Mhambe amefafanua kuwa, pia tayari kampuni 1,188 kutoka hapa nchini na 112 kutoka nje ya nchi zimethibitisha kushiriki maonesho hayo ambayo huwa yanavutia maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali.
Amesema, lengo kuu la maonesho hayo ni kuwakutanisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi na kuwapa fursa ya kutangaza bidhaa na huduma zao pamoja na kutafuta masoko mbalimbali.
Mbali na hayo amesema, katika maonesho ya mwaka huu yatakuwa na maeneo mbalimbali yaliyoboreshwa na programu za kuvutia ikiwemo ya Sabasaba Expo Village.
"Ili ni eneo ambalo limetolewa kutangaza fursa zilizopo katika sekta ya madini,Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), gesi na mafuta, siku ya mazingira, sanaa, vijana pamoja na wanawake,”amesema Kaimu Mkurugenzi huyo.
Pia ametoa wito kwa wafanyabiashara kushiriki katika maonesho hayo ya 47 pamoja na kutembelea banda maalum la SabaSaba Expo Village ili kuchangamkia fursa zilizopo na kuongeza kuwa hiyo ni nafasi nzuri kwa wajasiriamali kukuza na kujenga mtandao wa kuinua biashara zao.
“Hata hivyo Sabasaba Expo Village inatoa jukwaa la kujenga mtandao wa kibiashara kwa wafanyabiashara na kuwapa fursa ya kuanzisha mawasiliano na wenzao, kubadilishana uzoefu na kujenga ushirikiano mpya, eneo hili litawavutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wawekezaji, wafanyabiashara na wadau wengine wa biashara,”ameongeza.
Historia
Maonesho ya Sabasaba yalianza mwaka 1962 yakiwa ni maonesho ya kilimo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Wizara ya Biashara na Ushirika.Maonesho hayo yalikuwa na lengo la kukuza kilimo na ushirika.
Mwaka 1978, Serikali iliunda Bodi ya Biashara ya nje kupitia sheria yake namba 5 ya mwaka huo,bodi hiyo ilipewa mamlaka kushughulikia usafirishaji wa bidhaa za kitanzania nje ya nchi.
Bodi ya Biashara ya nje ilipewa pia dhamana ya kukuza ushirikiano wa biashara ya kimataifa kupitia maonesho ya kibiashara, kufanya utafiti kuhusiana na biashara.
Miaka ya hivi karibuni maonesho hayo yamekuwa yakishirikisha nchi mbalimbali kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), vilevile yamejulikana kama maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam na viwanja vinajulikana kama viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere.
Aidha, kwa mwaka huu wa 2023 kauli mbiu ya maonesho hayo ni "Tanzania Mahali Sahihi kwa Biashara na Uwekezaji" huku vionjo vipya vikitarajiwa kuyapa nguvu na heshima kubwa zaidi maonesho hayo ya Kimataifa nchini.
TWCC
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mwajuma Hamza amesema, wataendelea kuwawezesha wanawake kushiriki katika maonesho hayo ambayo yamekuwa ni chachu kubwa kwa washiriki wengi hasa kupata masoko ya uhakika.
Bi.Hamza amesema, maonesho hayo yamesaidia wajasiriamali wao kupata masoko ya uhakika, hivyo ushiriki ni mkubwa na wanawaahidi TanTrade kuwa wataendelea kuyatangaza maonesho hayo ambayo yanatoa fursa ya watu kujitangaza na kuuza biashara zao kwa wingi.
TCCIA
Akizungumza katika mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), Mwanahamisi Hussein amesema, wataendelea kuwaelimisha wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kushiriki maonesho hayo na fursa gani wanaweza kuzipata kwa lengo la kuinua biashara zao nchini.
Laizer
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Seasoning Palet (Tobi Product) ambayo inazalisha bidhaa zitokanazo na karanga, Agatha Laizer amesema, katika maonesho ya mwaka huu wanatarajia kuja na bidhaa bora zaidi.
Amesema, wanafanya hivyo kwa sababu Maonesho ya Sabasaba huwa yanatoa fursa kubwa kwa wajasiriamali ili kuweza kujitangaza na kuuza bidhaa zao.
“Kwa hiyo, niwatie moyo wafanyabiashara wenzangu hasa wale wenye biashara ndogo ndogo katika maonesho ya mwaka huu ya Sabasaba tuyatumie vilivyo ili kuendelea kutengeneza mtandao na kujitangaza zaidi.
"Tutakaposhiriki mwaka huu katika maonesho haya tutakuwa na uwezo wa kufanya kazi zaidi na kutengeneza mtandao mkubwa wa biashara ili kupata fursa mbalimbali zitakazotufanya tuzidi kuendelea mbele zaidi,”amebainisha Bi.Laizer.
Kwa nini TanTrade?
Hii ni taasisi ya umma iliyoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 4 ya mwaka 2009 yenye majukumu ya kuishauri Serikali kwenye masuala ya kuunda, kuendeleza, kusimamia na kutekeleza sera na mikakati za biashara nchini, kudhibiti na kutangamanisha maendeleo ya soko la ndani ya nchi na nje ya nchi.
Pia TanTrade ina majukumu ya kuzijengea uwezo Jumuiya za Wafanyabiashara juu ya namna bora ya kusimamia shughuli za biashara ya ndani na nje ya nchi, kuanzisha, kutunza na kuendeleza Kanzidata ya taarifa za biashara nchini pamoja na kuandaa na kuratibu Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yakiwemo maonesho ya viwanda, misafara na mikutano ya wafanyabiashara.