NA MWANDISHI WETU
Dar es salaam
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI) wameazimia kuungana kwa pamoja ili kuwezesha Maonesho ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania kuendelea kuwa yenye tija na yanayochochea uchumi wa mfanyabiashara mmoja mmoja pamoja na Taifa kwa ujumla.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Bi. Latifa Khamis akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Bw. Leodgar Tenga pamoja na Wataalamu wa pande zote kwa ujumla.
Kikao hicho pia kinaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha uchumi wa Viwanda unakuwa na kuongezeka kwa kasi zaidi, kwa kutangaza bidhaa za Tanzania pamoja na viwanda vya ndani ya nchi ili kuchochea uzalishaji na kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.