MSIMAMIZI wa Jimbo Katoliki Tanga Padri Thomasi Kiangio, anatangaza kifo cha Mheshimiwa Padri Francis Gembe kilichotokea tarehe 05/05/2023 katika Hospitali ya Bombo alipokuwa anapatiwa matibabu.
Misa ya mkesha itafanyika siku ya Jumatatu tarehe 08/05/2023 saa 11:00 jioni hadi asubuhi katika kanisa kuu la Mt. Antoni wa Padua- Chumbageni.
Na Maziko yatafanyika siku ya Jumanne tarehe 09/05/2023 saa 4:00 asubuhi Parokiani Kilole- Korogwe.
Habari ziwafikie Mapadre, Watawa wa kike na wa kiume, Viongozi wa H/W Jimbo, Waamini, Ndugu, Jamaa na Marafiki.
Apumzike kwa amani. Amina.