TCAA yatoa ufafanuzi kuhusu ndege ya Precision namba PW 602

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetoa taarifa kuhusu kugeuza kwa ndege Precision Air iliyokuwa inatoka jijini Dar es salaam kwenda jijini Dodoma siku ya Mei Mosi,2023 ikiwa na Kikosi cha Yanga ambapo imesema taarifa za awali za uchunguzi wa tukio hilo zimeonesha kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za kiuendeshaji.
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema, “Mnamo Mei 1, 2023 ndege ya Precision namba PW 602, iliondoka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA ), saa 12:11 jioni kwa safari ya saa moja kuelekea Dodoma ikiwa na abiria 72, ilitarajiwa kutua uwanja wa ndege wa Dodoma saa 01:13 usiku ambao ni muda zaidi ya masaa ya uwanja huo kufanya kazi.

“Uwanja wa ndege wa Dodoma hufungwa saa 12:30 jioni kutokana na changamoto za miundombinu zilizopo kwa sasa.

“Ilipofika majira ya saa 12:48 jioni Rubani wa ndege hiyo alilazimika kugeuza na kurudi uwanja wa ndege wa JNIA baada ya kushauriwa na muongoza ndege wa zamu, taarifa za awali za uchunguzi wa tukio hilo zimeonesha kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za kiuendeshaji.”

“Mamlaka inaendelea na uchunguzi wa kina kuangalia kama kuna uvunjaji wa kanuni za Usafiri wa Anga katika safari hiyo na endapo itabainika,mamlaka haitosita kuchukuwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

"Mamlaka inapenda kuuhakikishia umma kuwa uhairishaji wa kutua katika uwanja wa Dodoma ulifanyika kwa mujibu wa taratibu za usafiri wa anga zilizopo na katika muda wote si usalama wa chombo wala wa abiria angani uliokiukwa;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news