TRA yafanya maboresho makato kodi ya majengo kwa njia ya LUKU

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imetangaza viwango vipya vya kodi ya majengo vinavyokusanywa kwa kutumia njia ya ununuzi wa umeme kwa wamiliki. 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 4, 2023 na TRA, viwango vya utozaji kodi ya majengo kwa mujibu wa mabadiliko ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Kodi ya Mamlaka ya Serikali ya Mitaa (ukadiriaji), yaliyofanyika kupitia Sheria ya Fedha Na. 3 ya 2021.

Viwango hivyo vipya ni pamoja na, kiasi cha shilingi 12,000 kwa mwaka kwa nyumba ya kawaida shilingi 60,000 kwa mwaka kwa kila sakafu ya nyumba ya ghorofa katika maeneo ya majiji, manispaa na halmashauri.

Nyumba ya ghorofa katika maeneo ya halmashauri za wilaya, itatozwa kiasi cha Sh. 60,000 Kila mwaka.Awali, kiwango cha kodi hiyo ilikuwa shilingi 12,000 kwa majengo yote.

Taarifa ya TRA imesema kuwa, kwa sasa uhakiki wa majengo ya ghorofa unaendelea kufanyika na mita husika kuwekewa kiwango stahiki kulingana na aina ha jengo.

TRA inakusanya kodi hizo kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news