NA DIRAMAKINI
KURUGENZI ya Kipaumbele katika Upelelezi wa Uhalifu (Hawks) huko Limpopo nchini Afrika Kusini imeomba ushirikiano wa umma ili kuwabaini washukiwa wa ujambazi wenye silaha, wanaoonekana kwenye picha, baada ya walinzi wa G4S kuibiwa.
Limpopo ni miongoni mwa majimbo ya Afrika Kusini lililopo Kaskazini mwa Taifa hilo.Mji huo umepewa jina baada ya Mto Limpopo, ambao unaunda mipaka ya mkoa wa Magharibi na Kaskazini.
Msemaji wa Hawks huko Limpopo, Luteni Kanali Matimba Maluleke alisema Jumanne asubuhi kuwa, walinzi wa G4S walikuwa wakikusanya pesa kutoka kituo cha mafuta cha Global katika jumba la maduka la Big Boy huko Ga-Masemola na kuvamiwa.
“Walidaiwa kuvamiwa na watu watatu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto. Aidha inadaiwa kuwa washukiwa waliwanyooshea wafanyakazi hao silaha za moto na kuchukua begi la fedha likiwa na kiasi cha fedha ambacho hakikujulikana kutoka kwa walinzi kabla ya kukimbia eneo la tukio,”Luteni Kanali Maluleke alieleza. Majambazi hao wanadaiwa kutumia gari lao la kijivu aina ya Toyota Corolla.
"Kwa yeyote anayeweza kuwatambua watuhumiwa au kujua walipo anaombwa kuwasiliana na ofisa mpelelezi, Luteni Kanali Makutu kwa namba 071 481 2461 au WO Mojapelo kwa 073 261 8784," alisema Maluleke.
Awali, polisi huko Limpopo walitangaza kuwa wamewakamata washukiwa wanne na kuhusishwa na takribani visa 20 vya uvunjaji nyumba na wizi vilivyotokea katika mashamba katika eneo la polisi la Westenburg.
“Kwa mujibu wa taarifa, wakulima wa maeneo hayo wamekuwa wakikumbana na wizi mara kwa mara katika mashamba yao na watuhumiwa hawakuweza kufahamika. Hili lilikuwa jambo la wasiwasi kwao na polisi inaendelea kufuatilia kwa karibu,” msemaji wa polisi wa mkoa, Kanali Malesela Ledwaba alibainisha.
Alisema siku ya Alhamisi, polisi walipata taarifa kuhusu kundi la washukiwa ambao walidaiwa kuhusika na wizi huo uliokithiri katika jamii za wakulima ndani na karibu na Polokwane.
Washukiwa hao wanne walisemekana kuwa walikuwa wakiendesha gari kwenye barabara kuu ya N1 kuelekea Makhado.
Polisi mara moja walikusanya timu kutoka kitengo cha ujasusi wa uhalifu, kitengo cha ufuatiliaji, na kitengo cha kukabiliana na ujambazi ili kufuatilia tukio hilo.