NA MWANDISHI WETU
Arusha
WAKAZI wa Jiji la Arusha wameendelea kumiminika kwa wingi katika banda la Maonesho la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) katika Maonesho ya Pili ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) ili kupata huduma na ushauri wa kujiunga na mafunzo ya elimu ya juu.

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinaendelea kuwakaribisha wageni wote kutembelea banda la chuo hiki lililopo uwanja wa Sheikh Amri Abeid kupata huduma mbalimbali ikiwemo maelezo ya kukifahamu zaidi chuo, kozi zinazotolewa, udahili, mifumo ya ufundishaji na ujifunzaji, utafiti, huduma kwa jamii na ushauri wa Kitaalamu.
Nyote Mnakaribishwa