NA MWANDISHI MAALUM
WATU kadhaa waliokuwa wakisafiri na basi leo Mei 15, 2023 kutoka wilayani Mpanda mkoani Katavi kuelekea Mbeya wamenusurika kifo.
Ni baada ya basi walilokuwemo kutumbukia kwenye Mto Sitalike ambao ni maarufu kwa kuwa na idadi kubwa ya viboko majira ya saa 12:35 asubuhi.
Ajali hiyo imelihusisha basi la Kampuni ya Msingwa lenye namba za usajili T 441 DHZ ambapo chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kutaka kugeuza eneo lenye mlima kurudi nyuma.
Lengo ni kubadilisha njia baada ya kupata taarifa kuwa kuna gari limeziba njia eneo la Lyamba Lyamfipa. Taarifa zaidi zitakujia.