
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela, marehemu William Malecela aliyefariki dunia Mei 14, 2023, wakati Waziri Jafo alipofika nyumbani kwa Mzee Malecela Uzunguni jijini Dodoma leo Mei 16, 2023. (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS).