NA JOHN MAPEPELE
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe.Juma Zuberi Homera na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi wamefika kwenye Kijiji cha Mwanavala wilayani Mbarali kutokana na agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa la kuwataka kufika ili kuona hali ya ugomvi uliofanyika Mei 6, 2023 baina ya wananchi na wahifadhi pia mifugo liyokamatwa na kuuawa hali ambayo imethibitika kuwa hakuna kifo wala mifugo ilishikiliwa au kuuawa.
Hoja hiyo iliibuliwa juzi na Mbunge wa Mbarali, Mhe. Fransis Mtega aliyeomba kutoa hoja ya dharura ya kulitaka Bunge lijadili suala hilo hatimaye Waziri Mkuu kutoa maelekezo hayo ambapo jana ujumbe huo ulipata fursa ya kwenda na kukutana waathirika wa tukio hilo na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali na kufika eneo la tukio ambalo limebainika kuwa kilomita 20 ndani ya Hifadhi kwa mipaka ya awali na mita chache na kingo za Mto Ruaha.
“Nimesikitishwa sana na kauli za Mbunge ambapo baadhi ya malalamiko na shutuma zake dhidi ya Serikali zimeleta taharuki kubwa ambayo sijaikuta katika eneo hili na kwamba wananchi wamekiri kuingia ndani ya eneo hili na wameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa kuwatafutia maeneo ya kuishi,” amefafanua Mhe. Mchengerwa
Ametaja, baadhi ya tuhuma ambazo hazina ukweli na ambazo zimethibitishwa na wananchi wenyewe kuwa si kweli ni pamoja na wananchi kukataa kuwa hakuna mifugo iliyochukuliwa na wahifadhi 230 kama ilivyoripotiwa na Mbunge zaidi ya prukushani ya Mbwa wakali wa wananchi husika na wahifadhi, ambapo pia wananchi hao wamekiri kufanya shughuli zao ndani ya Hifadhi na wameomba wananchi hao kuzingatia sharia za uhifadhi hasa Sheria ya TANAPA.