NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nishati Mhe. Januari Makamba na watendaji wote katika Sekta ya Nishati kwa kuendelea kuhakikisha watanzania wanapata nishati ya umeme ambayo pia inasaidia katika uboreshaji wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
Waziri Ummy amesema hayo mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwenye maonesho ya Wiki ya Nishati inayoendelea kufanyika jijini Dodoma katika viwanja vya Bunge.
“Upatikanaji wa umeme wa uhakika unasaidia pia katika kuboresha huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa uharaka zaidi kwa kutumia vifaatiba,”amesema Waziri Ummy.