NA DIRAMAKINI
UONGOZI wa Wizara ya Afya umeeleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Dkt.Isack Sima aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyangoto kilichopo Wilaya ya Tarime Vijijini mkoani Mara.
Inadaiwa Dkt.Sima aliuawa Machi 3, 2023 kwa kukatwakatwa na mapanga na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake akitokea kazini.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 6, 2023 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya, Aminiel Buberwa Aligaesha.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Wizara ya Afya inalaani vikali kitendo hicho cha mauaji ya mwanataaluma ya udaktari na hakikubaliki katika jamii.
"Tunatoa pole nyingi kwa ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi, wanataaluma na watu wote walioguswa kutokana na mauaji haya.
"Tunawaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho Serikali kupitia vyombo vyake mbalimbali inafanya uchunguzi wa mauaji haya na itatoa taarifa mara tu baada ya uchunguzi kukamilika, pumzika kwa amani Dkt.Izack Sima,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Afya leo.