Wizara ya Afya yatoa maagizo kwa watumishi

NA MWANDISHI WAF

WAKURUGENZI na Waganga Wafawidhi wa hospitali za Taifa, Kanda na Mikoa wametakiwa kuwatia moyo na kuwahamasisha watumishi wa kada za afya kwenda kusoma maeneo yenye mahitaji ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi nchini.
Hayo yamesemwa leo na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo Wizara ya Afya, Dkt. Saitore Laizer wakati wa kufunga kikao kazi cha kuandaa mpango wa mafunzo ya kipaumbele kwa mwaka 2023/ 2024.

“Zoezi hili ni muhimu sana kwenye taasisi zetu hivyo tunaporudi kwenye maeneo yetu tujitahidi kuwahamasisha watumishi wetu waende kujiendeleza kwenye maeneo yenye uhitaji ili tuendelee kuboresha na kutoa huduma bora kwa wananchi wetu.”
Amesema, ufadhili wa masomo utatolewa kulingana na mahitaji yaliyopo katika kila hospitali hivyo mpango huo wa mafunzo utasaidia kuwa na watumishi wenye tija katika maeneo yote kwani Serikali imeweza kuboresha huduma za afya kwa kununua vifaa tiba vya kisasa pamoja na kuboresha miundombinu katika hospitali zote za Mikoa, Kanda na Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news