Wizara yasitisha mikopo ya wanawake kupitia WDF

NA DIRAMAKINI

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imetangaza kusitisha mikopo ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kupitia wizara hiyo leo Mei 28, 2023.

"Wizara inaujulisha umma kwamba imesitisha utoaji wa mikopo ya WDF. Hii ni kufuatia maboresho yanayoendelea kwenye utaratibu wa utoaji wa mikopo ya wanawake ikiwemo ile ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya kila halmashauri ambapo wanawake hupata asilimia 4.

"Lengo la usitishaji huu ni ili kufanya maboresho ya utaratibu utakaohusisha mikopo hiyo kutolewa na taasisi za benki.

"Utaratibu mpya utatangazwa punde utakapokamilika. Wizara inatoa rai kwa wanawake wajasiriamali waliopata mikopo kupitia mfuko wa WDF, kuendelea kurejesha mikopo hiyo kulingana na mikataba waliyosaini kati yao na wizara,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news