NA DIRAMAKINI
KOCHA Mkuu wa Yanga SC,Nasredeen Nabi amewataka wachezaji wake wakajitume ili washinde mechi ya kesho dhidi ya Dodoma Jiji FC.
Lengo likiwa ni kutawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo nchini.
Nabi amesema hayo leo Mei 12, 2023 kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC unaotarajiwa kuanza saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Kata ya Chamazi ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake,Afisa Habari wa Yanga SC,Ali Kamwe amesema, "Mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji ni mchezo muhimu na ndiyo mchezo wetu wa ubingwa.
"Ni mechi ya mwisho ya Yanga hapa Dar es Salaam, kesho ni sikukuu yetu ya kwenda kujipongeza kwa jasho lote tulilovuja msimu mzima, nawaomba mashabiki msije mkakosa kufika uwanjani.
"Mwenyezimungu akitujaalia tukashinda kesho,wachezaji wa Yanga watakuwa na tukio maalum la kuwashukuru mashabiki wote wa Yanga kwa kuwasapoti msimu mzima, hivyo tunawaomba mashabiki kesho baada ya ubingwa msiondoke,"amefafanua Kamwe.
Wakati huo huo,kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka Jumapili kwenda Rusternburg, Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji, Marumo Gallantssiku ya Jumatano katika Uwanja wa Royal Bafokeng.
Yanga itakwenda huko ikihitaji kuulinda ushindi wake wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Jumatano katika Uwanja wa Benjamín Mkapa jijini Dar es Salaam.
“Timu itaondoka alfajiri ya Jumapili, kesho tukitoka uwanjani baada ya Party tutakwenda sehemu tutapumzika kisha tutaanza safari ya kuelekea Afrika Kusini kucheza dhidi ya Marumo Gallants katika mchezo wetu wa nusu fainali.
“Tunamshukuru Mungu kwa kupata ushindi wa magoli mawili dhidi ya Marumo, lakini Wanayanga tusihadaike tukadhani shughuli imeisha, tuendelee kuoiombea dua timu yetu punde tu inapoanza safari ya kwenda Afrika Kusini,”amefafanua Afisa Habari wa Young Africans SC, Ali Kamwe
Mbali na hayo, Yanga SC inaongoza Ligi Kuu ya NBC kwa alama zake 71, ikifuatiwa na watani wao, Simba SC wenye alama 67 baada ya kuichapa Ruvu Shooting mabao 3-0 katika uwanja wa Azam Complex leo.