Yanga SC yatinga fainali Kombe la Shirikisho la Soka la Afrika (CAF)

NA GODFREY NNKO

KLABU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Tanzania imetinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) barani Afrika baada ya kuichapa Klabu ya Marumo Gallants F.C ya Afrika Kusini jumla ya mabao manne nyumbani na ugenini huku wakipata moja la kufutia machozi.
Leo Mei 17, 2023 wenyeji Marumo Gallants F.C ya Afrika Kusini imewakaribisha Yanga SC katika mtanange ambao umepigwa ndani ya Uwanja wa Royal Bafokeng nchini Afrika Kusini. 

Yanga SC wameshuka dimbani kuwakabili Marumo Gallants ya Afrika Kusini katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali Kombe la Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) wakiwa na mtaji wa mabao mawili ambayo waliyapata nyumbani.

Mchezo wa kwanza uliochezwa katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Yanga SC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa kipindi cha pili na Stephane Aziz Ki na Bernard Morison.
Kupitia mtanange huu wa marudiano leo, Yanga SC wameanza kuandika bao la kwanza lililowekwa nyavuni na Fiston Kalala Mayele dakika ya 46 katika kipindi cha kwanza.

Ni bao la ushindi ambalo lilidumu kipindi chote cha pili ambapo kipindi cha pili,Kennedy Musonda ndani ya dakika ya 62 alivuruga kabisa mipango ya Marumo Gallants F.C baada ya kupachika bao safi.
Kikosi hicho kiliwasili salama mji wa Rustenburg, Afrika Kusini siku mbili kabla ya mchezo huu na wakaanza maandalizi rasmi ya mchezo.

Aidha, Yanga SC haikusita kumshukuru Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi kwa maandalizi na mapokezi mazuri waliyoyapa kutoka kwa wananchi na watani wetu.

Kocha mkuu wa Yanga, Nasredine Nabi anatengeneza rekodi yake katika kikosi hicho baada ya kuwa na wakati mzuri tangu aliporithi mikoba ya Cedric Kaze ambapo hii ni historia ya aina yake kwa Wanajwangani hao ambao siku za nyuma walipitia katika kipindi kigumu.

Yanga inasubiria kukutana na mshindi kati ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast dhidi ya USM Alger ya Algeria.Bao la kufutia machozi la Marmo Gallants limefungwa dakika ya 91 ya mchezo huo na Ranga Chivaviro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news