Yanga SC yatinga nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imevunja rekodi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Ni baada ya Aprili 30, 2023 katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam kuambulia suluhu mbele ya wapinzani wao Rivers United kutoka nchini Nigeria.

Mtanage huo ambao ulikuwa wa kuvutia, kila pande ilionekana kutamani kuvuka hatua moja kwenda nyingine, lakini dakika 90 zilitamatika kwa pande zote ubao ukisoma 0-0.

Klabu ya Yanga wamefuzu kwenda Nusu Fainali kwa faida ya ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Nigeria, mabao ya mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele.

Aidha, Yanga SC sasa itamenyana na Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambayo imeitoa Pyramids ya Misri kwa jumla ya mabao 2-1, ikitoa sare ya 1-1 Cairo wiki iliyopita na kushinda 1-0 dhidi ya Phokeng, NW.

Wakati huo huo, Mechi ya kwanza Yanga na Marumo Gallants itafanyika jijini Dar es Salaam Mei 10, mwaka huu na marudiano yatafuatia Afrika Kusini Mei 17, mwaka huu.

Awali, katika mchezo huo Yanga ilifanya mabadiliko kadhaa ya nyota wake akiwatumia baadhi ya wachezaji ambao hawakuwa wanaanza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza kutokana na matokeo ya mechi ya kwanza kuwabeba.

Katika mchezo huo dakika ya 25, mchezo ulisimama kwa muda kutokana na hitilafu ya umeme kabla mambo kukaa sawa na mchezo kuendelea tena.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news