NA DIRAMAKINI
WATU watano akiwemo mtoto wa kike anayekadiriwa kuwa na miaka nane wamefariki dunia huku watu kadhaa wakijeruhiwa katika ajali ya basi la New Force namba T173 DZU.
Basi hilo linalofanya safari zake kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Rukwa limepata ajali baada ya kulipita kwa mbele lori na kuingia mtaroni katika Kijiji cha Igando Kata ya Luguda Wilaya ya Wanging'ombe Mkoa wa Njombe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, John Imori amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo majira ya saa nane na nusu mchana wakati basi hilo likiwa linatokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Rukwa.
"Kwa taarifa za awali basi la New Force lilikuwa linatoka Dar es salaam kwenda mkoani Rukwa, Sumbawanga lilipofika Igando kuna sehemu ya daraja likawa linataka kuovartake likapoteza uelekeo likaja wa likaingia mtaroni,” amesema Kamanda huyo.

Madereva wawe makini sana
ReplyDelete