Alizeti FC yaichanganya Utamaduni FC

NA ADELADIUS MAKWEGA

TIMU ya Mpira wa Miguu ya Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya (Utamaduni FC) imeondolewa katika nusu fainali ya mashindano ya mchezo wa soka baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penati minne kwa mitatu na timu ya Alizeti FC ya Mwitango Malya Kwimba Mwanza Juni 19, 2023 katika mchezo uliofanyika katika Viwanja vya Magereza Malya. 
Mchezo ulianza kwa chenga za hapa na pale ambapo dakika ya 23 ya mchezo huo mchezaji maarufu wa Alizeti FC Bukelebi Tomas alipunguza kasi wa washangiliaji wa Utamaduni FC na kuweza kuingia katika kumi na nane za lango hilo na kupiga mkwaju mkali ukaingia kimiani. 
Dakika ya 45 za kwanza ziliisha huku Alizeti FC wakitoka kifua mbele na hiyo ikiwa ni nyota njema uonekana asubuhi.
Alizeti FC
Hapo ndipo benchi la ufundi la Utamaduni FC liliweka mikakati kadhaa chini ya Ndinagu Sungura na wakarudi uwanjani kumalizia dakika 45 za kipindi cha pili na kurudisha bao na matokeo kuwa moja kwa moja. 
Waamuzi wa mchezo.

Mchezo uliendelea kwa pasi za hapa na pale huku kila upande ukishangiliwa ipasavyo na mashabiki wake na tambo za hapa na pale huku kukiwa na dalili za mikwaju ya penati. 
Hali hiyo ilisababisha viongozi wa Utamaduni FC kubadilisha golikipa wao Richard Kalinga na kumuingiza Subira Kaogisi ambaye anaaminika ni mzuri kuzuia mikwaju ya penati. 
Kweli dakika 90 zilipokamika matokeo yalikuwa moja kwa moja, hapo ndipo mikwaju ya penati ilipowadia ambayo Alizeti FC walipata penati nne nao Utamaduni FC walipata penati tatu..
Utamaduni FC

Hivyo Alizeti FC wameingia fainali watapambana na Black Mamba FC. Utamaduni FC wakipata penati tatu, matokeo hayo yamesaidia Alizeti FC kuingia fainali ya mchezo huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news