Balozi na Mtume Dkt.Peter Nyaga awashirikisha baraka watu wote kupitia Urejesho TV

NA DIRAMAKINI

BALOZI wa Kudumu wa Amani Duniani ambaye pia ni Mtume na Nabii Dkt.Peter Njue Nyaga wa Urejesho TV Africa na Kanisa la RGC Miracle Center lililopo Tabata Chang'ombe jijini Dar es Salaam amewaalika watu wote wakiwemo watumishi wa Mungu kushiriki kikamilifu kuchangia ujenzi wa studio ya Urejesho TV.
"Popote ulipo nchini Kenya waweza kutuma sadaka yako kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Urejesho TV kupitia Mpesa Kenya 🇰🇪+254 703 679 628 au ukiwa popte pale Tanzania waweza kushiriki baraka hizi za kujenga studio kwa kutuma sadaka yako kupitia Mpesa Tanzania 🇹🇿 +255 756 863 528. Ninaamini Mungu wa Mbinguni hatokuacha bure, na kila sadaka nitaitamkia neno la baraka, hivyo baraka zitaendelea kumiminika kwako,"amefafanua Balozi wa Kudumu wa Amani Duniani kote, Mtume Dkt.Peter Nyaga wa Urejesho TV AFRICA 🌍.

Wito huo anautoa ikiwa ujenzi unaendelea jijini Nairobi nchini Kenya kabla ya ujenzi mwingine kuendelea katika mataifa mbalimbali Afrika yakiwemo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huku Tanzania ikiwa miongoni mwa vipaumbele.
Mei, mwaka huu zilifanyika sherehe kubwa za kuadhimisha mwaka mmoja wa mafanikio ya Urejesho TV Afrika.

Urejesho TV Afrika inapatikana katika visimbuzi vya Azam TV, Zuku TV, Kwese TV, Nasa Tv, Muvi TV, Signet Kenya, Startimes Kenya na Go TC Kenya.

"Urejesho TV inapatikana kote ndani na nje ya Bara la Afrika, kwa Tanzania katika kisimbuzi cha Azam cha kufanya nenda other chanel,kisha nenda kwenye jina la Urejesho TV na kama hauipati sha kufanya sasa fanya auto search ikishamaliza kufanya auto-seach nenda other chanel, kisha chagua jina la Urejesho TV na ufurahie huduma zetu kwenye ubora wa hali juu,"amefafanua.
Mtume Dkt.Nyaga amebainisha kuwa, Urejesho TV ni kati ya runinga bora zaidi duniani ambayo imekuwa ikirusha matangazo mubashara kote barani Afrika na duniani kwa ujumla huku lengo likiwa ni kuzidi kuifikia jamii kwa karibu zaidi na kutangaza neno la Mungu.

Amesema, makao makuu ya runinga hiyo yapo nchini Kenya ilipojengwa studio yake ya kwanza na wanatarajia kujenga nyingine hapa Tanzania.

“Pia,tunataka kufungua studio hapa Dar es Salaam ambapo studio namba moja ipo Nairobi nchini Kenya,namba mbili itakuwa hapa,namba tatu nchini Rwanda,namba nne nchini Burundi tutakwenda hivyo mpaka tufikie nchi saba,“alisema Mtume na Nabii Dkt.Nyaga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news