Bandarini tuliache, penye kasoro pafanyiwe maboresho twendeni huku-Mwinjilisti Temba

NA DIRAMAKINI

MWINJILISTI wa Kimataifa, Alphonce Temba ambaye ana uzoefu wa kuishi katika mataifa zaidi ya 10 duniani yenye bandari zilizowekezwa huku matokeo chanya yakionekana kwa ustawi bora wa Taifa na jamii, ameshauri mambo kadhaa ili kuongeza ufanisi katika sekta ya bandari nchini.

"Hivi karibuni nilitoa clip inayozungumzia masuala ya bandari, nadhani nilikuwa wa kwanza, baada ya Bunge kuidhinisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

"Baada ya hatua ile, mjadala ulikuwa mpana zaidi hasa kwa upande wa Serikali, tukaona baadhi ya viongozi wakizungumza akiwemo Msukuma, tukamuona Waziri Mkuu pamoja na Msemaji wa Serikali Msigwa (Gerson Msigwa) cha ajabu mjadala unazidi kukuwa na unanishangaza.

"Kinachonishangaza zaidi kuhusu mjadala huu wa Serikali ni pale Serikali ilichelewa kutoa awareness kabla, sasa wamerekebisha wanafanya, kuna watu wanazunguka sasa na hizi taarifa ambazo zinatolewa na Waziri Mkuu akiwemo Msemaji Mkuu wa Serikali, na viongozi wengine mbalimbali.

"Kuna taarifa nyingine ambazo zinakuja kwa nguvu hasa kwa ndugu zetu wanaotokea Bukoba (mkoani Kagera) bila kujua kuna muunganiko gani ya watu wazito kutoka Bukoba kupinga, na hata kuhoji kwamba sasa kwa nini kulikuwa hakuna ushindani,sasa hivi unaweza kuhoji, lakini pia watu wanahoji mambo ambayo sasa yanatolewa ufafanuzi, kwamba hiki kitu kipo hivi na hiki kipo hivi.

"Na wengi, hawajawahi kuzungumza hata siku moja, mimi nimekuwa nikizungumza mara kwa mara kuhusu masuala ya bandari kwa miaka 10, nimeishauri Serikali iwekeze nguvu kwenye bandari kavu huko Kwala, nimeishauri Serikali iweke mzani huko Vigwaza, nimeishauri Serikali ijenge border ya Tunduma zaidi ya miaka 10 hadi 12 na imekuwa ikifanya.

"Sasa tunapokuja hadharani kuzungumzia masuala ya bandari, siyo kwamba tunakuja kimihemko, hapana na Serikali ituone sisi watu ambao tunayazungumzia haya na iyafanyie kazi.

"Lakini, ikianza kusikiliza kila Mtanzania kuhusu huu mpango, kuna watu ambao wamepandikizwa kwa ajili ya huu mpango kabambe wa kuvuruga Serikali,Serikali tulishaipa dhamana ya kura, iongoze nchi na si kila jambo ambalo litakuwa linafanywa na Serikali tutalijua mapema, Nyerere (Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere) halipokwenda kusikia habari ya kelele za nchi kuingia katika mfumo wa vyama vingi au la,

"Lakini, matokeo ya kura yalionesha asilimia 80 walikuwa hawataki, ni asilimia 20 tu walikubaliana na huo mfumo akajiongeza kuwapa wale wenye asilimia ndogo kwa wakati tena kwake binafsi ambapo iliwashangaza na kwa sababu tu kulikuwa hakuna vyombo vya habari huenda kungekuwa kuna mjadala kama uliopo leo.

"Kwa sababau pia aligundua ni bora tujiandae mapema, tuingie kwenye huo mfumo, sasa kama leo Seikali kuna mambo ambayo inayafanya hayana madhara na inaona umuhimu wake ila kuna marekebisho ambayo yanapaswa kufanyika, kama nilivyoishauri Serikali, na Waziri Mkuu alisema kutakuwa na maboresho kila baada ya miaka kadhaa.

"Kitu nilichokizungumza mimi na kuishauri Serikali, Waziri Mkuu ameshakijibu, sasa mimi ninadhani tuiache Serikali ichape kazi, tuleteeni Mwarabu apige kazi, tunamuhitaji Mwarabu aje afanye kazi, mpeni Kwala, Mwarabu mpeni bandari Mwarabu na tunataka mizigo yote iishe bandari kavu Dar es Salaam, tunataka msongamano na malori yaishe.

"Bandari ya Kurasini haitakiwi, Bandari ya Kwala inatosha mizigo yote tuishauri Serikali sasa ni nini cha kufanya kuhusiana na bandari, ukiweka bandari Kurasini bado mchezo wa wizi utakuwepo, toa bandari kuu na kituo cha mwisho kiwe Kwala, mizigo yote kuanzia sasa ikiwemo ya Tanzania kuwe na incharge atakayekaa bandari kuu na incharge bandari kavu Kwala.

"Incharge wa bandari kuu anakusanya taarifa zote zinakwenda Kwala, Kwala wanakuwa wanatoa huduma kwa maana ya taratibu za kiserikali , TRA wanaangalia vilivyotoka bandari kuu ya Dar es Salaam na vilivyoingia Kwala na vilivyotoka kwa wananchi hapo kazi kwisha.

"Na Mwarabu anakaa pale, Mwarabu mmeshamscreen hawezi kufanya chochote cha usanii, wapigaji hawapigi, TPA haifanyi chochote kibaya badala yake mambo yanakwenda.

"Zaidi ya hapo, Serikali tutaipasua vichwa na mjadala huu hautaisha, tunahitaji Mama (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan) usaini mkataba kama haujasaini watu waingie kazini.

"Wapo watu ambao ni 'majayanti' wanafahamika na nina clip zaidi ya 200 namna gani ambavyo nimeizungumzia bandari zaidi ya miaka 15, mimi ndiyo mtu ambaye nimeizungumzia zaidi kwa sababu ninajua ninachokizungumza, siyo kwamba mtu anakurupuka tu kutoka huku na kule, hapana.

"Awe Mbunge, awe Sheikh, Mchungaji awe nani njoo na data, no data no research no right to speak, hauna data, hauna vielelezo hauna uhalali wa kuwaeleza watu vitu, utawaeleza kwa data gani?.

"Kwa hiyo, ninaishauri Serikali kwa moyo mkunjufu wamefanya jambo jema, tunahitaji uharaka, nchi inahitaji fedha, matozo yamekuwa mengi angalau Serikali ije ipangilie mambo maisha yawe mazuri, huu mkoa wa Pwani kuna baadhi ya maeneo hayana barabara ya lami hata kilomita kumi na sasa hivi umekuwa ni mkoa wa kiviwanda.

"Ni mkoa wa kibiashara, ni jiji la kibiashara kama huko Kwala vimechukuliwa vijiji mpaka kule Mzenga vijiji 30, Chalinze Peramumbi, Mzenga vimekuwa ni eneo la kibiashara kunatakiwa kupasuliwa mabarabara kutoka Kwala kwenda Mzenga kwenda Kisarawe.

"Treni ya umeme, watu watoke Dar es Salaam waende kule kwa nauli ya shilingi 1,500 tu, unalipia tiketi ya treni ya umeme kwenda kule dakika 10 hadi dakika 20 wafanye kazi warudi tuhamishe mji wa Dar es Salaam umekuwa mkubwa, mambo ni mengi vijana wamekuwa wengi hawana kazi, ajira zaidi ya milioni moja watu wakapate huko Kwala na sehemu nyingine.

"Hivyo ndivyo vitu Serikali inatakiwa iviangalie, umuhimu wa haya na Kwala kuanza, tunajua Kwala imekuwa na ucheleweshaji muda mrefu, barabara imekwisha kamilika kutoka Vigwaza hadi Kwala kilomita 15 isipigwe na jua tena barabara ikapasuka.

"Tunahitaji malori yaende yakachukue mizigo, maeneo ya Kwala na Mabala yatengenezwe, vitengenezwe vitega uchumi mbalimbali yakiwemo maduka hawa Wakongo au Wazambia wakirudi hawana haja ya kurudi tena Kariakoo wanaishia kule kule.

"Tunauhamisha mji kimipango, kiuchumi na Halmashauri ya Chalinze ninaishauri ipime kuanzia Chalinze, Pingo Chamakweza, Mbala, Ruvu, Vigwaza, Buyuni, Nafco wapime mji vizuri watuwekee hata hekari moja barabarani ya bustani kama ilivyo Mnazi mmoja sehemu ya mapumziko .

"Kwa sababu, mji hauwezi kuwa tu ni nyumba nyumba hauna barabara za kutoka, barabarani kuanzia Vigwaza hakuna njia ya kutoka nje watu wamejenga sheli na yadi tu barabarani kuwepo na njia ya za mita 30 kuingia ndani. Hii ndiyo mipango sasa watu waishauri Serikali, what's way foward watu wanamuona tu Mwarabu?.

"Mimi, Alphonce Temba,Mwinjilisti wa Kimataifa tumelimaliza kuanzia leo, tuendee kutoa ushauri wetu na michango juu ya namna gani kule kuendelezwe ili watu waende kule wafanye kazi.

"Ninawapongeza, wafanyabiashara wa Tabata Dampo tayari wameshakwenda Vigwaza wameshanunua zaidi ya hekari 150, sasa hivi wanajenga, wamepeleka mpango miji wanatengeneza barabara.

"Wanatengeneza kule kwa ajili ya shughuli zao, watu wanaokwenda bandarini, viongozi wa vijiji, Mwenyekiti wa Kijiji cha Daraja Ruvu, Darajani kuna viwanja vinatolewa kule kwa bei nafuu sana hadi laki tatu, 20 kwa 20.

"Ili wananchi mbalimbali waende kuwekeza wajenge kule nyumba, Mwenyekiti wa Kijiji cha Vigwaza kwa Zoka, Mwenyekiti wa Kijiji cha Vigwaza Kambini,Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mlindi tayari wana fursa. Mwenyekiti wa Buyuni, Mwenyekiti wa Vishezi wananchi nendeni kwenye ofisi za wenyeviti mpakate maeneo yenye fursa huko.

"Kwa sababu kuna malori zaidi ya elfu 20 ambayo yatabaki Vigwaza mapaka Chalinze mpaka Mzenga ambayo madereva watahitaji nyumba za kupanga, watahitaji hoteli hivi ndiyo vitu vya kuzungumza sasa vya kiuchmi siyo yada yada ya kurudi na DP World, DP kazi yake tulishaimaliza tunamuhitaji haraka nimuombe Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan asikilize maneno yangu na ushauri ninaoutoa, kwa kweli nilitoa ushauri huko nyuma.

"Mimi ndiye nilitoa ushauri ijengwe bandari kavu Kwala na mzani wa Vigwaza mwaka 2008 nilimuandikia barua aliyekuwa Waziri Mkuu mwaka 2019, Mheshimiwa Mizengo Pinda nikamuelezea umuhimu wa mzani kuondoka Kibaha kwenda Kwala kwa sababu ya foleni na masuala mengine ya kiusalama.

"Ili pia kuondoa msongamano wa malori mjini, miji yote duniani hakuna mji unaoruhusu malori yaingie mijini ovyo kama yanavyoingia Dar es Salaam.

"Miji yote duniani, malori yanaingia mijini kwa vibali tena usiku kushusha mizigo tu, siyo kila mahali malori yanatapakaa, ikumbukwe kuna malori yanatoka Congo, yanayotoka Angola, yanayotoka huko Zimbabwe na kwingineko kuna magonjwa kama Ebola ambayo yanaweza kutembea pia katika mavumbi mbalimbali.

"Wanavyoleta hayo malori sijui kuyaosha Tabata au sehemu mbalimbali sijui Mbezi tunaweza hata Watanzania wakapata maambukizo ya magonjwa, kwa hiyo ndiyo maana hayo malori hayatakiwi kuingia au kujaa kwa wingi yanapotoka safari na ndiyo maana ukiingia nchi kama ya Zambia.

"Nimekaa zaidi ya nchi 13 nina uzoefu mkubwa, unakuta malori yanapita mahali ambalo ni eneo lililotengenezwa kwa kuwekwa maji ya dawa, yanapuliziwa dawa ukiingia Botswana, ukiingia Namibia, ukiingia South Africa na ukiingia Zimbabwe kasoro Tanzania tu ndiyo sijaona.

"Mahali ambapo tunafanya hivi vitu, kwa sababu malori yanapotoka na mavumbi na magonjwa ya binadamu au ya wanyama yale magonjwa yanadhibitiwa kabisa, lakini Tanzania hatuna leo tunaruhusuje malori kuingia kwa fujo namna hiyo, ikifika jioni saa moja kuoka Ubungo kuja mpaka Mbezi malori msongamano ni mkubwa wa malori wakati watu wengi wanatoka makazini.

"Wakati haya yanatoka kwenda Congo, nyakati nyingine asubuhi ukija pale Temboni unakuta pale Kibanda cha mkaa unakuta malori yamezuiliwa pale yasiingie na yana vumbi nyingi sana yametoka nayo huko Congo na ndiyo maana watu wanapata magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kansa.

"Na ikiwezekana ufanyike utafiti na watu wa mazingira wakaangalia na ikiwezekana hilo vumbi lipimwe ili iweze kubaini iwapo vumbi linalotoka mataifa mengine ni salama au limebebeba magonjwa kwa sababu hatufanyi treatment yoyote.

"Haya ndiyo mambo bunifu, mambo ya udadavuzi, mambo uniques ambayo tunapaswa tuyazungumze, siyo masuala ya mjadala wa Mwarabu tena, hayo tumeshayamaliza bungeni, na Serikali hii tuiunge mkono kazi, ikiprove failure ndiyo tunawaambia saa leo tunawakalia kooni wakati tumewapa nchi, halafu iweje?.

"Na kwa nini tusimamie jambo moja, hakuna mambo mengine yanaonekana ni makosa ni hilo tu peke yake?Hapana, tunafanya makosa, Serikali mmeshasikia, ushauri wangu kwa Serikali vile vitu ambavyo vimepigiwa kelele hasa mkataba utakavyowekwa muwe makini na muwakaribishe wapinzani pia wanasheria wao waje waangalie katika kuendeleza kama kuna umuhimu huo.

"TLS wapo pale waende wataalamu wabobezi wa sheria, watusaidie ili jambo tuachane nalo, yada yada hatutaki tumekwisha maliza, Watanzania tupo tayari na tunaiunga mkono Serikali, binafsi ninaikubali na kuisapoti Serikali kwenye jambo hili na nitasimama kama Balozi bila hata kupewa na Rais wala Waziri Mkuu kwenye hili,asanteni," amefafanua kwa kina Mwinjilisti wa Kimataifa Alphonce Temba leo Juni 26,2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news